017: KIPINDI CHA MASHAKA


why such a long face?

I am sorry to break the news but unfortunately, I don't have the desirable content for my audience. The blog is struggling to remain relevant to the majority of its readers.

Watu wengi wanaosoma blog hii,kwa sasa wanataka kusikia juu ya mambo ambayo sina uzoefu,busara wala mamlaka ya kuyazungumzia.
Unajua, hadhira yangu kubwa ni watu na hasa marafiki zangu nilionao rika moja....
Sehemu kubwa ya rika hili, ndio inaanza rasmi kuingia kwenye kipindi cha mashaka maishani mwao.

Kipindi hiki kimetawaliwa na tamaa za kutisha,mabadiliko ya kushangaza na maswali mengi yasiyo na majibu ya Ndio/Hapana.
Si rahisi kuyajibu!
 
Nitapataje kazi?--Napataje pesa?
Nikizipata niwekeze kwenye nini?
Nikaishi mkoa/nchi gani?
Nitajuaje mchumba niliyenae ananifaa?-Au nampataje ikiwa sina?

Baada ya miaka kadhaa ya balehe kali iliyotuaminisha tunajua kila kitu na tusiambiwe chochote na yeyote; Kipindi cha mashaka kinapoingia,tunaanza kutaka kuuliza tufanye nini na tufanyaje,tena tuelekezwe step by step.
 
Alas! wapo pia wanaoanza kuogelea kwenye dimbwi la ndoto walizoota kwa muda mrefu na wanamashaka kama ndio dimbwi lile lile walilolipima joto lake kwa kidole na kina chake kwa kijiti na wakaridhika.
Walipodumbukia rasmi kupiga mbizi,wanaona kila kitu kimezidi.
Joto linataka kuwaunguza na kina kinataka kuwazamisha.
Watoke haraka au waendelee kuvumilia na hatimaye watazoea?

Wengine wanapambana kukubali kupotezeana na marafiki waliowahi kuamini watakuwa wa kufa na kuzikana miaka fulani nyuma.
Unajua kipindi cha mashaka ni wakati unaokuja na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa yanayoweza kuathiri vibaya mmea wa urafiki🌴
Lazima pande zote zinazohusika kuutunza, ziwe tayari kujaribu mbinu mpya za kuulea. Ikitokea upande mmoja ukalegea au zote mbili zisijali, mmea huu utasinyaa na kujifia🍂.

Ndio,pande hizo hazitokuwa maadui lakini maongezi yao hayatokuwa ya furaha kama zamani. Kuna uchungu watauonja kwenye ndimi zao kila wanapozungumza. Hatia ya kuua mti mzuri ambao si rahisi kuustawisha tena;haijawahi kuwa na ladha nzuri mdomoni mwa yeyote.
 
Sasa blog hii inatembelewa zaidi na watu wa rika hili.
Watu wenye maswali mazito ambayo nasita kujaribu kuyajibu mahali hapa.
Watu wanaotaka kuambiwa cha kufanya lakini hawana experience ya kutumia neno "nifanyaje?"
Watu wanaopaswa kuanza kurasa mpya lakini bado hawana utayari wa kufunika zile za zamani...

Wanategemea niweke lolote la kutusaidia kwenye blog hii wakati ambao mimi pia 
sina cha kusema kwa sababu ni mwenzao😵
Ni mara yangu ya kwanza pia kuingia kipindi hiki cha mashaka. Ninamashaka kwa kila jipya linaloendelea mahali hapa. 
Nakosa cha kuwaelekeza wengine kwani itageuka simulizi ya vipofu wanaoongozana njia. Si punde wakaanza kutiliana shaka.
Safari yao ikawa ya shaka juu ya mashaka,yaani shakashaka 😂😂😂
 
Lakini mashaka haya yasituzuie kutiana moyo wa kusonga mbele,kupeana mkono wa kushika na bega la kuegamia katika kipindi hiki. Hii ndio imani yangu!
 
Ikikupendeza, usisite kuacha ujumbe mfupi na mzuri hapa chini kwa watu wote waliopo kipindi cha mashaka hata kama wewe pia ni mmoja wao…Inawezekana si rahisi kuwaelekeza wengine kushughulika na yale ambayo binafsi pia yanatusumbua lakini inafariji kujua kuwa husumbuliwi peke yako😄

I would truly appreciate having a collection of some positive messages down here.
I think above all, that is the desirable content my audience needs.

A gentle reminder of Hope!

A hope that eventually time will bring the best answers to all the questions, doubts, and worries we harbor right now,
.……….and all will be but history!
 
With gratitude for life,
Auxanus
@DeChambu

Comments

  1. 🙌🏻This is so relatable.I think my message of hope will be from Joshua 1:9📍

    ReplyDelete
    Replies
    1. "Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako"

      Delete
  2. This is a bittersweet composition.inanihuzunisha afu ikiona nakaribia kulia inanichekesha😂😂💔
    To contribute to the collection,I would advise to avoid over consumption of other people's lives especially through social media.
    You might think you're being inspired but there's a danger of being depressed and pushed to a negative comparison.
    Please limit social media.It will make the pressure filled years a bit easier to navigate

    ReplyDelete
  3. Tukaze💪

    ReplyDelete
  4. Long time no see brother.nimefurahi umerudi tena😁
    Mimi naomba wkt wa mashaka tusisahau kusikiliza Three Little Birds by Bob marley and the wailers 🫶🏼 It works every time

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hey Anonymous, you know I know you 😂😂. Thank you!

      Delete
  5. Ni kipindi kigumu nimepoteza hamu ya mambo mengi niliokua nikiyapenda najaribu njia mpya nikiamini kupata matokeo tofauti ila njia nipitazo zimejaa mashaka😕

    ReplyDelete
  6. Cornel kakokoJanuary 21, 2024

    Tutayaweza yote katika yeye atutiae nguvu, kwa msaada wa Kristu tutayatenda makuu. On our hardest times we should always remember to wake up and keep blue flag flying high.🫂

    ReplyDelete
  7. Keep doing it, he always has a trick up his sleeve, GOD

    ReplyDelete
  8. Umri huu ni wa maswali mengi sana kwakweli.
    Japo, katika kila shaka tulilo nalo tukumbuke tu kuwa mwisho wa siku 'Maisha ni kitu aali' 🙂 na Mungu ni mwema siku zote. Kila kitu kitajipa tu ✊🏾
    Naomba utupe maana ya aali kaka Dechambu kwenye reply hapo chini😅

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts

001.MWANZO

015: UGUMU WA URAHISI

016: SALA YA KUOMBA KIFO CHEMA.

014: KUHUSU MAKOMWE

013.CHASING WEMBLEY

012.KIPAJI SI UMAARUFU WALA PESA

005.KUNJUA MKONO