001.MWANZO

πŸŒ„Mwanzo.

[WaShaRaRaaA,Picha Linaanza....πŸŽ₯πŸ˜‚]

Si mwanzo kwa maana ya kuanza ila kwa maana ya hatua mpya katika muendelezo.

Kwa mfano,tunaambiwa kuwa wakati fulani Mungu aliumba mbingu na dunia: na tumeamua kuutambua wakati huo kama ndio mwanzo. Lakini tunaamini kuwa alishakuwepo tangu milele.

Au wapendanao wanaoridhia kuoana baada ya kipindi kirefu cha kuchumbiana.Unakuwa ndio mwanzo wa ndoa yao japo tunafahamu kwa hakika kuwa wanahadithi kabla ya siku ile.

Kwa hiyo mwanzo huu pia ni mwanzo kama huo. Haujaanzia hapa.

Niseme nimekuwa nikiandika-andika kwa muda mrefu kidogo. Nimeandika hadithi, makala fupi, mashairi na risala.Kama unamchumba ambaye ni rafiki yangu,inawezekana kuna barua uliwahi kuipokea kutoka kwake na kumbe niliiandika mimiπŸ˜‚ na namdai hajanilipa!πŸ’”.

Juzi,nikaamua nianze kuandika machapisho yatakayokaa mtandaoni na ndio ukawa  mwanzo wa Blog hii.

Ninapenda kuandika.Ninaona kunanipa nafasi ya kutazama maisha kwa karibu zaidi:jinsi yanavyopita na kutembea huku na kule.Ninafurahi pia kuona baadhi ya watu wanaonizunguka wanapenda kusoma niyaandikayo. Hivyo natazamia Blog hii kuwa sehemu nzuri ya mimi na wao kukutana,kila mmoja kwa nafasi yake.

Niwe muwazi kuwa nimeshawahi kushauriwa kuifungua au kufikiria kufanya hivyo mimi mwenyewe lakini sikutilia maanani. Wakati mwingine ningejikatisha tamaa na kusemea moyoni "Hakuna watu wanaosoma Blog siku hizi".
Ulikuwa mchanganyiko wa woga na uvivu.

Lakini hivi karibuni nilipotembelewa tena na wazo lile:nilijikuta nikilikaribisha ndani na kulipikia chakula bila kuwaza mara mbili.Sijui ni kwa nini ila ninapenda kuamini kwamba huu ndio umekuwa muda sahihi kufanya hivyo.Kuna sehemu pia ukifika kwenye maisha yako, huogopi tena kama utapata watu au la. Unataka tu kufanya vitu ulivyoahirisha kuvifanya kwa siku nyingi.
Nahisi sasa hivi ndio naishi mtaa wa karibu na hio sehemu.
Kama na wewe unatamani kuja kuishi mitaa hii, usisite. Niambie nikutafutie chumbaπŸ˜‚

Ta-da! Here is the Blog I have always procrastinated to create....😁

Mji huu mdogo unaitwa nothing-specifick kwa sababu hauhusu kitu kimoja kinachoeleweka.
Ningependa kuandika kuhusu chochote ninachoweza. Juu ya maji na mawe. Mambo ya kweli na ya kufikirika.Nilioyaona na ninayoyasikia. Mziki, nyota, safari na wanyama. Matukio yaliyonigusa, mapya ninayojifunza na ninavyochukulia baadhi ya mambo.
Kwa lugha ya kiswahili,kiingereza or a touch of both!

Kwa jamaa yule nisiyemfahamu,ambaye nilisoma makala yake mtandaoni akishauri ni vyema Blog yoyote ijikite katika suala moja maalumu ili itambulike kirahisi,anisamehe kwani sitofuata ushauri wake mzuri kwa sasa.
Kutambulika ni ndoto ninayoweza kulala bila kuiota kwa miezi.Lakini kuandika chochote ninachotaka ndio furaha inayonikurupusha usingizini.

Utagundua kuwa nothing-specifick ina '-' katikati na 'k' mwishoni.Imenipasa kuviweka kwani yupo aliyeniwahi  jina hilo katika usahihi wake tangu mwaka 2004 (nikiwa chekechea😹)
And as ironical as it may be,the nothingspecific blog has nothing as of today!
Hivyo ukiwa unakuja mji huu, uwe makini na anwani hio.Usije ukapotea na kuingia mji mwingine ulio kimya na tupu.
Labda jina hilo linaweza kubadilika huko mbeleni lakini hivi sasa ninauhakika ndio nalitaka.Raha ya kuwa mwanzoni mwa jambo, ni uhuru wa kuliweka inavyokupendeza.

Juu ya yote,nimshukuru kila mmoja aliyekuwepo kabla ya mwanzo huuπŸ™
Aliyewahi kusoma chochote nilichoandika na kukipenda au kukikosoa.
Familia yangu na marafiki zangu wasiochoka kusoma madubwasha yanguπŸ™ˆ
Kama umesoma hadi huku, basi wewe pia ni mmoja wao!

Nimalize kwa kukukaribisha sana mahali hapa.Ukipata muda,pitia usome yatakayokuwemo kuhusu nothing specific....
Yanaweza kukufurahisha,kukupa moyo au kuboresha mtazamo wako juu ya maisha.
[Unaweza pia kusubscribe kwa email ili ushtuliwe kukiwa na mapya ya motoπŸ”₯πŸ˜‚]

Mlango utakuwa wazi muda wote.Unaweza kuingia na kutoka kadri utakavyo.
Jisikie upo nyumbani!πŸ˜‰

With nothing specific,
Auxanus Chambulila.
@DeChambu.

Comments

  1. AnonymousMay 05, 2023

    Wonderful

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2023

    Perfect

    ReplyDelete
  3. Mdaiwa suguMay 05, 2023

    Sawa unanidai malipo ya barua tangu Fm2 lkn ndo uniandike kwenye Blog??πŸ˜‚

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2023

    An artistic side of being an introvert 😎

    ReplyDelete
  5. Kuna chakula cha wageni mtaa huu jameniπŸ˜‚. This is very good thinking keep it up Mr. Chambu

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 05, 2023

      nothing specific just napita πŸ˜‚

      Delete
  6. AnonymousMay 05, 2023

    Someone once said
    "The noblest art is that of making others happy..".
    Keep it up man.πŸ‘πŸ‘

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 11, 2023

    Amazing

    ReplyDelete
  8. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kijana upate tofali mia tatu kama pongezi!

    ReplyDelete
    Replies
    1. πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ™πŸ»Naomba nipate na supu ya yule kiumbe aisee!πŸ˜†

      Delete
    2. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ af kweli, nadhani ndo ilikuwa siri ya ushindi kuzimaliza tofali 300

      Delete
  9. AnonymousJune 01, 2023

    πŸ˜‚πŸ˜‚

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2023

    Safari ya to "nothing specifick." πŸšΆπŸ˜‚

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts

015: UGUMU WA URAHISI

017: KIPINDI CHA MASHAKA

016: SALA YA KUOMBA KIFO CHEMA.

014: KUHUSU MAKOMWE

013.CHASING WEMBLEY

012.KIPAJI SI UMAARUFU WALA PESA

005.KUNJUA MKONO