015: UGUMU WA URAHISI

"Moto hauzai moto;Huzaa majivu"

Uhitaji wa huduma ya matibabu ya kupangilia meno unazidi kushika kasi duniani. Sasa ni kitu cha kawaida kupishana na kijana aliyevaa Braces mdomoni.

Kwenye kitabu chao cha Jaws: The Story of a Hidden Epidemic, Bi.Sandra na Bw.Paul wanalitazamia suala hilo kama matokeo ya urahisi wa kutafuna.

Miaka mingi nyuma,meno ya binadamu yalikabiliwa na kazi kubwa ya kusaga vyakula vigumu.Baada ya watu kuongezeka ujanja, tumeweza kupika na kusaga misosi hadi ikawa laini kabisa.

-Matokeo yake?🤔

Meno na taya zilizotengenezwa kufanya kazi ngumu, hazifanyi tena hivyo. Zimebaki kuzubaa na hatimaye kuanza kuparaganyika kinywani.
Wanyama wengine wafananao nasi,mathalan Nyani; hawapitii changamoto hiyo sana kwa sababu hawana uwezo wa kuinywa ndizi ikiwa katika umbo la mtori.

Juhudi za binadamu kurahishisha kutafuna chakula, zinaishia kumuingiza gharama ya kutembea na vyuma mdomoni.

Taratibu,tunaanza kuona kuwa urahisi katika maisha huja na ugumu wake. 

Unajua miaka ya 1820+, wanafunzi wa hesabu walihimizwa kushika hadi Table ya 50 kwa kichwa.
Urahisi wa Calculator na Multiplication Tables nyuma ya Daftari, haukuwepo.
Leo tunahimizwa kushika hadi Table ya 12 tu lakini muulize mwanafunzi 9 x 8 na usishangae aki-load.
Kuna confidence, mental stimulations na math skills za muhimu zinatupotea watu wa kizazi chetu.

Si ajabu baada ya miaka mingi ya kutumia Chatgpt na wenzake,ipo siku tutashindwa kufanya kazi bila kuwategemea.Si tu kwa sababu ni njia rahisi kukamilisha mambo ila itakuwa ni dhahiri HATUWEZI kufikiria majibu sahihi au mazuri kwa kichwa.

Ukiwa na njia ya haraka ya kutatua changamoto fulani, akili na mwili vinalala.Unarelax.Hasa pale ambapo  unauhakika njia hiyo inapitika.

Natumaini umewahi kusikia watu wakisema kuwa watoto wa matajiri hawajui kutafuta maisha (pesa)

Kuna wakati nilikuwa nafikiri wazo hilo ni sehemu nyingine ya chuki za chinichini za wasionacho lakini ninavyozidi kuishi, ninanusa kaharufu ka ukweli ndani yake.

Vijana wanaoweza kupiga simu nyumbani wakiishiwa fedha, hawajui kuzitafuta.
Ndio, wanaweza kuanzisha shughuli za kujitafutia kipato na zikafanikiwa lakini kuna stress muhimu wanaikosa.Kichwani wanatambua hata wakifeli, hawato lala njaa na wanaweza kuanza tena upya.

Asiye na wa kumpigia,hana hio luxury.Anajua akijichanganya kidogo tu atalia na kusaga meno.
Anapania.
Kuwa makini ukishindana naye maana hutofurahi ukijua yupo tayari kufanya nini ili akushinde.

Kusingekuwa na mchezo wa “KAMLETE”, kuna kila dalili vijana wengi wanaotokea kwenye familia zenye uwezo kifedha, wangetabika kustahimili soko la ushindani.

Upo mtego wa kupitia njia rahisi kwani mara nyingi huishia kutuacha kwenye njia panda ngumu.

Sisemi tuziache wala sichochei tuzifuate bali najiuliza kama tunaweza kuwa nazo makini au zimeumbwa kutunasa?

Swali hilo nakuachia wewe pia!

Comments

  1. AnonymousJune 09, 2023

    Big up brother , nimejifunza kitu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2023

    Sad reality

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 10, 2023

    Nilikuwa na mpango wa kuweka na mimi 😂😂😂

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kawahi kuweka😂meno yanahitaji support😆

      Delete
  4. AnonymousJune 10, 2023

    I see the way you use your brain perfectly brother rather than waiting for Chatgyt. You deserve to be father of Modern World writings

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2023

    Agreed!!!

    ReplyDelete
  6. Matarlou LubangoJune 10, 2023

    This is great enlightment.. Congratulations @Mr. DeChambu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts

001.MWANZO

017: KIPINDI CHA MASHAKA

016: SALA YA KUOMBA KIFO CHEMA.

014: KUHUSU MAKOMWE

013.CHASING WEMBLEY

012.KIPAJI SI UMAARUFU WALA PESA

005.KUNJUA MKONO