005.KUNJUA MKONO
Mzoea kutwaa,kutoa ni vita!
![]() |
| Kunjua mkono 📸: Rawpixel |
Kutenga muda kutushauri⌚
Kutukopesha bila kutudai-dai,💰
Kutuunganishia mishe za kufanya,👷
Kutusalia au kutupa company nzuri inayoongeza furaha na amani kwenye maisha yetu ♡
Ni majukumu wanayoyapata automatically tu ila kusema ukweli wanastahili malipo.
~Japo kidogo.
Kweli upo duniani kwa miaka 20+ na hujawahi kumnunulia Mama hata Khanga au Baba hata Soksi:Unasubiri utoboe!🤔
~Tobo which? Tobo How?
Wengine hadi bila kujua tunawaombea watu wanaotusaidia matatizo ili tupate nafasi ya kuwalipa wema wao. Utasikia, “Huwa ananisave sana.Akipata shida ya pesa nitampa hata yangu ya kula”
~Vipi asipopata?
Kunjua Mkono. Hakuna aliyemasikini kiasi kwamba hana cha kutoa.
Siku mjazie mshkaji wako kabandle ka-aftatu📱
Mnunulie shosti kilemba cha kulalia🧣
Muandikie Uncle nia ya misa kumuombea afya📿
It can be simple:Sio hadi ubebe Dunia uwape!
Usiendekeze kusubiri apate shida sijui utoboe,maisha hayatabiriki.
Unaweza ahirisha kulipa hizo fadhila kila siku kwa kusema kesho,keshokutwa na ukaishia kumlipa shada la maua.
People aren't here forever.
And even if they are,uzoeshe mkono wako kukunjuka.Ukikazana sana kuukunja,kuna siku utapata hiko unachosubiria ila utashangaa haukunjuki.
Mazoea hujenga tabia.
Na tabia ni kama ngozi.Kuivua,yatakutoka machozi!

Comments
Post a Comment