016: SALA YA KUOMBA KIFO CHEMA.
Kiimani, mimi ni Mkristo na katika sehemu fulani ya maisha yetu ya utoto, tunapaswa kuhudhuria mafunzo maalumu ya dini. Nadhani ni utamaduni wa kawaida maana hata wenzetu Waislamu huenda Madrasa.
Nikiwa na miaka 10, nilikuwa katika mafunzo hayo na siku moja tukajifunza kuhusu “Sala ya Kuomba Kifo Chema”
Nilikuwa naifahamu sala ile. Nilishawahi kuisikia mara kadhaa nyumbani bali sikuwahi kuelewa hasa ni nini kinachoombwa. Siku tulipojifunza, ndio akili ikanifunguka na sikuhisi amani sana kuisali😒
Nilikuwa naifahamu sala ile. Nilishawahi kuisikia mara kadhaa nyumbani bali sikuwahi kuelewa hasa ni nini kinachoombwa. Siku tulipojifunza, ndio akili ikanifunguka na sikuhisi amani sana kuisali😒
Sasa ni zaidi ya miaka 10 imepita na hisia zangu hasi juu ya sala ile zimepungua makali lakini hazijawa butu. Huwa ninaisali kwa kujikunja kwani kuna namna inanifinya utumbo.
Kwenye utamaduni wa Kiswahili kuna kitu kinaitwa Uchuro au Uchimvi.
Hii ni pale unapofanya au kusema kitu kinachoashiria jambo baya hasahasa kufa.
Kwa mfano, mkiwa mnakula pamoja na wenzako kisha ukajifanya umekabwa na kuanza kutapatapa.
Wakifahamu unatania it is likely watakwambia “Acha Uchuro!”
Uchuro ni mbaya na tunafundishwa kuuepuka tangu tukiwa wadogo.
Tunahimizwa kuugopa.
Ninavyozidi kuishi na kukua, ninaona unintended consquences nyingi za kuogopa uchuro.
Watanzania (labda na wengine wenye tamaduni za kufanana nasi), tunashindwa kufanya mambo kadhaa ya muhimu vizuri kwa sababu tu yanatufanya tujihisi tunachuria.
Nina mifano mingi ya mambo hayo na mmoja wapo ni ile hofu yangu ya kusali sala ya kuomba kifo chema. Nimegundua sala ile inanifinya utumbo kwa sababu msingi wake ni uchuro.
Kijana mdogo nawazaje kufa?!
👴Babu yangu anayekaribia miaka 90, anaisali kwa amani na sauti ya juu zaidi.
Kuna siku nilipanda gari ambalo rafiki yangu ndiye alikuwa anaendesha✇
Baada ya kukaa, nikajifunga mkanda na hapo hapo akaniuliza kwa utani ulioonekana kukosa ladha ya mzaha, “Vipi! Humuamini dereva?”
Nikakenua kwa ukakasi😀
Kwenye macho ya tuliokuzwa katika tamaduni zinazoamini uchimvi, kufunga mkanda ni kujichuria. Nadiriki kusema Gari lingekuwa ni ugunduzi wa Mtanzania, lisingekuwa na mikanda.
Hatupendi kuitumia huku tukisingizia inatubana nk ila chini ya haya yote imejificha imani ya uchuro inayotusuta kila tunapotaka kujizungushia zile kamba.
Watu wanapata vilema vya maisha,wengine wanayapoteza na kuharibika sura na maungo hata ndugu zao wanashindwa kuwaaga vizuri kwa sababu tu waligoma ‘kujibana’ na mkanda.
Waliogopa kujichuria ajali.
Unataka Mzee wako akose usingizi?--Tafuta muda umuulize ameandaa vipi masuala ya mirathi ikitokea ametangulia.
Anaweza hata akakulaani!😂
Lakini kuna mifarakano mingi ya kifamilia ingeepushwa iwapo watu wangezoea kuandika wosia.
Ila familia kibao hazijawahi kuzungumzia mada hio kwa sababu ni kukaribisha nuksi.
Mhoji M-Bongo typical ameenda lini hospitali kwa ajili ya general check-up?
Atakushangaa na kukujibu tusi linalotamkwa “Hayo ni mambo ya Kizungu!”
Kwenda kukagua Afya wakati HUHISI kuugua si sehemu ya mazoea yetu kwani ni aina fulani ya uchuro.Hata wahudumu wa Hospitali wanaweza kukubeza.
“Unahamu ya kuumwa wewe?!”
Hatimaye tunaishia kuchangishana kwenda India huku wengine wakipoteza vizazi au utimamu kwa matatizo ambayo wangekuwa na mazoea ya check-up, wangeyawahi.
Muda mwingine nadhani ndio maana tunapata tabu sana kushughulikia matatizo/majanga yanapotokea. Ajali,mafuriko,vimbunga nk.
Tamaduni zetu hazituruhusu kuamini katika kujiandaa kuyakabili.
Kikosi cha zimamoto🚒 kinachelewa kufika eneo la tukio kwa sababu kilianza KUTAFUTA maji BAADA ya kupigiwa simu kuwa “Huku Kumewaka!”
Kukaa na maji ya kuzimia moto kwenye gari ni uchimvi.Tena ingekuwa ni maamuzi yetu, hivyo vikosi visiwepo kabisa.Tunajichuria ajali za moto kwa kuwa navyo😹
Nilijifunza sana wakati wa msiba wa ♛Malkia Elizabeth kwa kusikia kuwa itifaki ya msiba wake ilipangwa tangu mwaka aliosimikwa. Taratibu zote za nani atatangaza kifo,watapita mitaa gani na kuishia wapi, zilikuwa zinajulikana miaka 70 kabla ya tukio lenyewe kutokea.
Usikute hata kundi fulani la viongozi wakubwa waliopandishwa kwenye Bus walipohudhuria msiba ule, ilikuwa ni sehemu ya utaratibu ulioandaliwa mwaka 1952, miaka kabla hata ya nchi zao kupata uhuru!
Kuandaa itifaki ya msiba wa Malkia, hakukumua Bi.Elizabeth. Ila kulisaidia sana mazishi yake kuwa tulivu na yenye utaratibu.
Kikosi cha zimamoto🚒 kinachelewa kufika eneo la tukio kwa sababu kilianza KUTAFUTA maji BAADA ya kupigiwa simu kuwa “Huku Kumewaka!”
Kukaa na maji ya kuzimia moto kwenye gari ni uchimvi.Tena ingekuwa ni maamuzi yetu, hivyo vikosi visiwepo kabisa.Tunajichuria ajali za moto kwa kuwa navyo😹
Nilijifunza sana wakati wa msiba wa ♛Malkia Elizabeth kwa kusikia kuwa itifaki ya msiba wake ilipangwa tangu mwaka aliosimikwa. Taratibu zote za nani atatangaza kifo,watapita mitaa gani na kuishia wapi, zilikuwa zinajulikana miaka 70 kabla ya tukio lenyewe kutokea.
Usikute hata kundi fulani la viongozi wakubwa waliopandishwa kwenye Bus walipohudhuria msiba ule, ilikuwa ni sehemu ya utaratibu ulioandaliwa mwaka 1952, miaka kabla hata ya nchi zao kupata uhuru!
Kuandaa itifaki ya msiba wa Malkia, hakukumua Bi.Elizabeth. Ila kulisaidia sana mazishi yake kuwa tulivu na yenye utaratibu.
Nasikia hadi nyuki wake aliokuwa akiwafuga, walipewa taarifa kuwa mtawala wa Kasri hayupo tena.
Maskiniii! Itakuwa walilia sana huko mizingani 🐝💔
✅ Ifike mahali turuhusu baadhi ya uchuro kwenye maisha yetu.
Tukubali kuzungumzia na kupanga vizuri juu ya masuala yasiyonoga kuyavutia picha.
Wewe ni mwanachuo kama mimi?-- Tenga hela kwa ajili ya SUP mwezi wa 9😹😂
Hutoipata kwa sababu umetenga hela. Lakini ukiipata, unayo fedha tayari.
Itakuepushia fedheha ya kuanza kupiga simu na kueleza watu changamoto yako ili wakukopeshe bajeti ya kuja kufanyia mtihani.
Binafsi nataka kujifunza kuishi na mauchuro kadhaaa.
Nataka kufunga mkanda kwenye Gari,
Nataka kwenda general check-up Hospitali.
Nataka kuweka hela kwa ajili ya siku ninazoweza kuzihitaji ghafla.
Nataka pia kuandika wosia. Si wa mali ila wa nyimbo😁😂
Kuna nyimbo ambazo si za dini na ningependa zipigwe muda watu wanakula ubwabwa baada ya kunipumzisha.Najua nisipoelekeza, hazitopigwa.
Watapiga tu yale manyimbo machungu anaimba M-Baba fulani hivi...😆
Kuna Mauchuro ni sawa na kusali Sala ya Kuomba Kifo Chema 🙏🏻
Haikuui ila inaahidi kukufanyia msaada siku yako inapofika.
Hatutofikwa na mabaya kwa sababu tumejiandaa kuyakabili.
Lakini yakitufika, yatatukuta tunapakuanzia……
'Gari lingekuwa ni ugunduzi wa Mtanzania lisingekuwa na mikanda' 😂😭😂 I died
ReplyDeleteNimesoma hili andiko nikiwa nacheka kama vile nilikuwa najua kipi unachenda kukisema😂 I appreciate kwa sababu always unakuwa na mawazo ya kutaka kubadilisha baadhi ya mazoea , ila mh !! Kujichia kaburi kabla hujafanya pagumu apo😂 any way nitabadilika mana na mm naonaga ni uchuro
ReplyDeleteIt's interesting to me that umegusia some of Tanzanian’s norms ambazo nazifahamu ila labda ningeshindwa kuzi-point out in an obvious way. I’m glad now you have come to the point of seeing the importance of saving
ReplyDeleteKwenye general check-up inabidi tubadilike kwakweli, afya ni kitu aali😅😅
ReplyDeleteLeo nimeelewa kwanini kuna baadhi ya vitu vizuri tunavikwepa kufanya. Itabidi tubadilishe mwenendo, haiui bali inaandaa...😁
umenigusa kwenye uchuro wa "wosia part" 😂 I was half-half before reading this, I now admit kuna baadhi ya uchuro inabidi tuushi.. thanks for paving ways always
ReplyDeleteKaka hapo kweny kutenga pesa kwa ajili ya SUP mwezi wa 9 🙌🙌😹
ReplyDelete