012.KIPAJI SI UMAARUFU WALA PESA

Mtu hupata ajaliwalo,si alitakalo.


🎭🎨💰😎

Siku hizi watu wenye vipaji tunaongoza kwa stress za kupata Viewers👀,Likes👍 & Comments💬 mtandaoni.
Tunamhaho wa kuvuna fedha na umaarufu kupitia vipaji vyetu😰

Sure! It’s a good thing, so if you are confident you have the talent, take chances.
Tuoneshe kipaji chako kwa nguvu na kujiamini.
ILA ufanye ukifahamu kwa hakika kuwa kuna mawili.
1. Tukupende,tukulipe na tukufanye uwe Super Star!⭐
    AU
2.Tuishie kukushangilia na kukupigia makofi halafu tusitoe hata thumni na tusikufuatilie tena.

Unajua anayetoa vipaji si mchoyo. Amehakikisha kuwa vipo vingi sana huku Duniani. Changamoto ni kuwa jamii haiwezi kumlipa na kumtukuza kila mwenye nacho😐
Huwa inachagua wachache wa mfano, inawapa hela na umaarufu kwa niaba ya wengine wanaopaswa kwenda kulima ili watu wale😋.
Inauma,lakini kubali utakapodondokea.
La sivyo utaishi maisha yako yote ukiwa na uchungu moyoni kuwa watu hawakusapoti au wanakuwekea vizingiti.
Kumbe badala ya kuwachomea nyama wajilambe,wewe unakazana kuwaforce wanunue picha ulizochora hao wanyama😆

Tupunguze kupanick na kulalamika.
Let's just look at talents for what they really are; God-given abilities to guide us as we find meaning and joy in life, not necessarily to gain fame and money with.

The truth is you have higher chances of making a dime by selling to people rice, sugar or medicine than waiting for them to pay you for making their heartbreaks less lonely with your songs!

Unahaki na wajibu wa kwenda kutafuta hela sehemu nyingine nje ya kipaji chako.Kwa kutumia nguvu💪,akili 🧠 au vyote kwa pamoja.
Lakini jitahidi utenge muda wa kukiishi,kukifurahia na kuwashirikisha wengine ili wakifaidi,hasa siku za ujana wako.
It makes you feel alive and blessed💫
Mashabiki na tuzo ni by-the-way tu!

Hata aliyetupa hizi talanta SIDHANI kama swali lake KUU litakuwa ni tuliingiza nazo shilingi ngapi.

Ila labda atasema ‘Nilikupa kipaji cha kuchonga,nioneshe vinyago vyako!

Sasa je, unacho cha kumuonesha?
Mwenzako sitaki stress, nitampa hii Blog aipitie chap kwa haraka!😂

Comments

  1. AnonymousMay 16, 2023

    I feel attacked 😂 thanks for this truthful article

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts

001.MWANZO

015: UGUMU WA URAHISI

017: KIPINDI CHA MASHAKA

016: SALA YA KUOMBA KIFO CHEMA.

014: KUHUSU MAKOMWE

013.CHASING WEMBLEY

005.KUNJUA MKONO