014: KUHUSU MAKOMWE
Je wajua?
Yamkini limezidi au kupungua. Na uwezekano mkubwa ni hapo kwenye kuzidi๐
Of course,unahitaji kifaa ili kupima.Na kifaa hiko ni vidole vyako vya mkono.
![]() |
| ๐ธ:Kupima Komwe |
Kwa kawaida komwe la mtu huwa sawa na vidole vyake vinne vya mkono. Unaweza kutumia vidole vya mkono mmoja au vya mikono yote miwili,yaani kidole cha shahada na cha kati kwa kila mkono.
Ukiona unaviweka kwenye komwe na nafasi pana inabaki, hapo ujue kuna dalili komwe lako limechukua nafasi kubwa zaidi ya inavyopaswa.
But we can enjoy for the fun of it!
Unajua kuna muda utani unamuingia mtu!
Wengi tunafahamu ya kwamba kuna sehemu za miili yao (wadada) zinakuwa na ukubwa au mbinuko wa ziada. Ukimuuliza mtu yeyote azitaje sehemu hizo, haraka atasema kuhusu MaHips na Kifua kwa sababu zimeandikwa kwenye mada ya Ukuaji, kitabu cha Sayansi darasa la 6.
Thanks to that,it is now a common knowledge that women are naturally curved ()
Lakini tafiti zinaonesha kwamba inawezekana na komwe ni miongoni mwa sehemu hizo ila tu ilipuuzwa au kusahaulika.
Wataalamu wa sura na mifupa wanaeleza kuwa kwa wastani, makomwe ya wadada ni curved kuliko ya wanaume. Kuna namna yamebinuka zaidi na ni mbinuko huo unaosaidia kutofautisha sura ya kiume na ya kike miongoni mwa tofauti nyinginezo.
Sasa mahali pakibinuka,patakuwa na ukubwa fulani hivi…
Kuna uelekeo kwamba bila kujua: wanaume huvutiwa zaidi na wadada wenye makomwe yanayojidhihirisha kuliko yasiyo๐.Komwe lililonawiri ni miongoni mwa viashiria vya wazi kuwa Binti ni mwenye siha njema na amepevuka.
Upo uwezekano pia kuwa hata kusuka au kufunga vilemba kumekuwa utamaduni wa kike sehemu nyingi duniani kama sehemu ya jitihada za kuonesha makomwe yao. Misuko mingi ya nywele, inazivuta nyuma na kuacha nafasi ya komwe kuonekana kubwa kuliko uhalisia wake.INALIKUZA bila ya kuliongeza๐.
Ni kama tu mdada anavyovaa suruali ya kubana ili kuonesha Shape inayoweza isiwe bayana sana kwenye Sketi ya Marinda.
Ubaya wa “uzuri” ni dhana ya kutengenezwa na watu wenyewe na hivyo inabadilika.Kuna siku waliamka wakaapia “Black is Beautiful” lakini waliporudi usiku kulala,wakasema wadada weusi ni wachawi ๐น๐
Kwa hiyo hata makomwe yanaweza kupitia mabadiliko hayo.Wakati fulani yakapendwa na muda mwingine yakapondwa.
I know it's a clichรฉ lakini kitu cha msingi kwa yeyote ni kujifunza kujiamini na kujikubali jinsi alivyo.Sehemu kubwa ya maumbile yetu,it is non of our doing!
At the end of the day,ukubwa au udogo wa komwe hauna uzito sana kushinda kilichomo ndani yake.
Unaelewaje mambo?
Unafaa kuwa Mama anayeweza kuwaelewesha mambo hayo vizuri watoto wetu?
Chukua hatua!
Haki Makomwe…!๐
๐Nge nge!


๐๐ hatua whic’
ReplyDelete๐
ReplyDelete๐๐๐ปChambu unachokitafuta utakipata
ReplyDelete๐๐๐๐
ReplyDelete
ReplyDelete๐๐