015: UGUMU WA URAHISI
"Moto hauzai moto;Huzaa majivu"
Uhitaji wa huduma ya matibabu ya kupangilia meno unazidi kushika kasi duniani. Sasa ni kitu cha kawaida kupishana na kijana aliyevaa Braces mdomoni.
![]() |
Kwenye kitabu chao cha Jaws: The Story of a Hidden Epidemic, Bi.Sandra na Bw.Paul wanalitazamia suala hilo kama matokeo ya urahisi wa kutafuna.
Miaka mingi nyuma,meno ya binadamu yalikabiliwa na kazi kubwa ya kusaga vyakula vigumu.Baada ya watu kuongezeka ujanja, tumeweza kupika na kusaga misosi hadi ikawa laini kabisa.
-Matokeo yake?🤔
Wanyama wengine wafananao nasi,mathalan Nyani; hawapitii changamoto hiyo sana kwa sababu hawana uwezo wa kuinywa ndizi ikiwa katika umbo la mtori.
Juhudi za binadamu kurahishisha kutafuna chakula, zinaishia kumuingiza gharama ya kutembea na vyuma mdomoni.
Taratibu,tunaanza kuona kuwa urahisi katika maisha huja na ugumu wake.
Urahisi wa Calculator na Multiplication Tables nyuma ya Daftari, haukuwepo.
Leo tunahimizwa kushika hadi Table ya 12 tu lakini muulize mwanafunzi 9 x 8 na usishangae aki-load.
Kuna confidence, mental stimulations na math skills za muhimu zinatupotea watu wa kizazi chetu.
Si ajabu baada ya miaka mingi ya kutumia Chatgpt na wenzake,ipo siku tutashindwa kufanya kazi bila kuwategemea.Si tu kwa sababu ni njia rahisi kukamilisha mambo ila itakuwa ni dhahiri HATUWEZI kufikiria majibu sahihi au mazuri kwa kichwa.
Ukiwa na njia ya haraka ya kutatua changamoto fulani, akili na mwili vinalala.Unarelax.Hasa pale ambapo unauhakika njia hiyo inapitika.
Natumaini umewahi kusikia watu wakisema kuwa watoto wa matajiri hawajui kutafuta maisha (pesa)
Kuna wakati nilikuwa nafikiri wazo hilo ni sehemu nyingine ya chuki za chinichini za wasionacho lakini ninavyozidi kuishi, ninanusa kaharufu ka ukweli ndani yake.
Ndio, wanaweza kuanzisha shughuli za kujitafutia kipato na zikafanikiwa lakini kuna stress muhimu wanaikosa.Kichwani wanatambua hata wakifeli, hawato lala njaa na wanaweza kuanza tena upya.
Anapania.
Kuwa makini ukishindana naye maana hutofurahi ukijua yupo tayari kufanya nini ili akushinde.
Kusingekuwa na mchezo wa “KAMLETE”, kuna kila dalili vijana wengi wanaotokea kwenye familia zenye uwezo kifedha, wangetabika kustahimili soko la ushindani.
Upo mtego wa kupitia njia rahisi kwani mara nyingi huishia kutuacha kwenye njia panda ngumu.
Sisemi tuziache wala sichochei tuzifuate bali najiuliza kama tunaweza kuwa nazo makini au zimeumbwa kutunasa?
Swali hilo nakuachia wewe pia!
.jpeg)
Big up brother , nimejifunza kitu
ReplyDeleteSad reality
ReplyDeleteSure
ReplyDeleteNilikuwa na mpango wa kuweka na mimi 😂😂😂
ReplyDeleteKawahi kuweka😂meno yanahitaji support😆
DeleteI see the way you use your brain perfectly brother rather than waiting for Chatgyt. You deserve to be father of Modern World writings
ReplyDeleteAgreed!!!
ReplyDeleteThis is great enlightment.. Congratulations @Mr. DeChambu
ReplyDeleteThank you Brother 🙏🏻
Delete