011.UNAJUA NINI?

Msikiti usio na maji,hauswaliwi!

"Unajua Nini?"


Kwa kawaida ili watu wakulipe fedha,upate riziki ya kuendesha maisha yako ni lazima uwe na kitu unachomiliki au kukifanya [vizuri] ambacho wao hawafanyi.

Aidha hawakiwezi,hawakijui au hawana muda lakini wanakihitaji.

 

Sasa Mimi na rafiki zangu wengi tunaosema “Tutafute Hela” hatujui kufanya kitu chochote [vizuri].

Na kusema ukweli hatuhangaiki sana kujifunza kwa nia wala bidii.

Kubwa tunalofanya ni kujenga maghorofa hewani. Na kisha kuilalamikia awamu iliyopo madarakani na mfumo wetu wa elimu kwamba maghorofa hayo hayajengeki kwa sababu yao😁

 

Tunachosomea shuleni/vyuoni hatujui vizuri kwa hio tegemeo letu kuu la ajira ni serikali.

Ikitangaza sandakalawe,tudake yetu!

Nje ya hapo ni undugu🧬 au ujuzi🧠

Sasa kama huna ndugu wa kukubeba,kila usiku kabla hujalala inabidi ujiulize unajua nini?

 

Wengi wetu ukituuliza,tunajiuma-uma tu kwa aibu.

-Kiswahili “Nimemkuta Hayupo”

-English |You’re Vs Your| Loose Vs Lose| Borrow Vs Lend|  ni Headache-Causative.

-Shika PC uEmpty recycle bin; Jasho la kwapa!

-Unaujua mtishamba wa kupunguza homa?- Hapana.

-Biashara isn't your thing.

-Kusuka,kunyoa,kushona-Kimya!

-Kadi yako ya chama inamuda gani?-Huna

-Na kuhusu kulima ulishasema over ‘you’re’ dead body!

 

Unaamini umebobea kwenye matumizi ya Instagram,Tiktok nk ila ukiambiwa umsaidie mfugaji kuvitumia kufanya digital marketing ya bidhaa zake, ndio unaanza kujua kuwa inawezekana hujui vizuri😢

 

Labda basi hujali ya Dunia kwani ni ya kupita;

Basi tuongoze kuswali Tarawehi🕌, Hujui.

Tuanzishie wimbo wa Roho Mtakatifu🕊 tufungue ibada, Huujui.

Shika kibuyu uite maBabu👵👴 zako, Huwajui.

 

Sasa unajua nini?🤔

Ndio changamoto zipo na ujuzi pekee si silaha inayoweza kuzimaliza lakini angalau ni risasi salama ya kuanzia.

Jiulize vizuri,Unajua Nini?

Na je,watu wanakihitaji kiasi cha kuwa tayari kukulipa vihela ili wakipate?

Kwa maana usikute unachojua ni changamsha genge tu kama hii Blog.Siku nitakayowaambia watu walipie💸 kuaccess hizi content, ndio utakuwa mwanzo wa kuzisoma mwenyewe!😭😂

 

Comments

  1. AnonymousJune 23, 2023

    😅😅siku utakayowaambia walipe izi content utakuwa mwanzo wasome wenyewe🙌...
    Anyways nimejifunza kitu apa👊

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts

001.MWANZO

015: UGUMU WA URAHISI

017: KIPINDI CHA MASHAKA

016: SALA YA KUOMBA KIFO CHEMA.

014: KUHUSU MAKOMWE

013.CHASING WEMBLEY

012.KIPAJI SI UMAARUFU WALA PESA

005.KUNJUA MKONO