010.JISAMEHE

Ukimficha jogoo pakachani,kuna muda atawika!


 "Yaishe!"

Tangu tukiwa wadogo, tunafundishwa kuomba msamaha tukiteleza na kuwasamehe wanaotukosea.
Kuna namna tunakuzwa na wazo la kwamba “Msamaha ni lazima ukuhusishe wewe na mwingine”
 
Lakini mengi tunajikosea wenyewe na tunabaki kuteseka miaka nenda rudi kwani kujisamehe si kitu tunachofahamu kama kinawezekana au hata kipo duniani.
Kuna mtu hadi leo amekuwa mkubwa na anafamilia ila bado anajichukia kwa kuleta mvua kitandani akiwa ugenini darasa la tatu.
 
Inatesa😖

Ukiona cheti cha Form 4 unahisi uchungu. Unaamini ungekuwa serious kidogo zaidi ile F ingekuwa C😞
 
Ex alikuomba msamaha kwa kukudanganya kuwa hakuna zaidi yako baada ya kugundua kuwa yupo. kisha kila mtu akashika njia yake kwa amani ila kuna siku hulali ukijiuliza kwa nini ulimpenda na kumuamini?😔
 
Kuna watu umewakwaza na wamesamehe ila wewe bado hujajisamehe kwa kuwakosea na haipiti wiki bila moyo wako kukukumbusha kuwa unaumia juu ya hilo💔
 
Asubuhi uliambiwa amelazwa ila kuna kauvivu ukakasikia na ukasema kesho utaenda kumuona. Usiku ukapigiwa simu kuwa hayupo tena. Miaka imepita lakini ukikumbuka unatamani kujichapa na mkanda😫

Umewahi kujiomba msamaha?
 
Wengi tunaishia kuwa na hasira, hofu na mood swings kibao.
Makosa yetu binafsi yanatuwinda na badala ya kusimama kidete kupambana kujisamehe, tunakimbilia kujificha kwenye kichaka cha “No regrets, Just Lessons” bila kusahau kile cha “Everything happens for a  reason.”

Hii inanikumbusha hadithi ya mbuni, aliyeficha kichwa na kuacha mwili wote ukionekana.Lakini kwa sababu kwa kufanya vile akawa hawezi kumuona moja kwa moja anayemuwinda, basi akaamini kuwa na muwindaji hatomuona pia.

"No Regrets,Just Lesson"


Kichaka hiki cha quotations kinatupa faraja ya muda tu ila baada ya muda,tunagundua kuwa tumeonwa na ugomvi unazidi kuwa mkubwa.
 
Sifahamu vizuri kinachoweza kufanyika kwani mimi si mtaalamu wa masuala hayo lakini ni muumini wa kutulia.
Ukiniulize tufanyaje, basi wazo langu la kwanza ni kuwa TUTULIE.

Tukubali makosa na tujiombe radhi taratibu.
Ikiwezekana tujiadhibu kwa kufunga,kufanya usafi mwingi na kutafuta tunayeweza kumuamini na kumshirikisha hio “aibu”. Inadhoofika ikujua tumepata ujasiri wa kuitamka kwa mwingine.

Tuweke jitihada za kujisamehe.
Si rahisi ila INAWEZEKANA💫.

Comments

Post a Comment

Popular Posts

001.MWANZO

015: UGUMU WA URAHISI

017: KIPINDI CHA MASHAKA

016: SALA YA KUOMBA KIFO CHEMA.

014: KUHUSU MAKOMWE

013.CHASING WEMBLEY

012.KIPAJI SI UMAARUFU WALA PESA

005.KUNJUA MKONO