009.WAKUJA & KIDUARA

Mgeni ni kipofu,ingawa anamacho yake!

*Hadithi hii ya 'Wakuja & Kiduara' iliandikwa mara ya baada ya fainali za Kombe la Dunia 2022.

Sayari ya Wakuja ikionekana kwa mbali.
[Najua hujaiona😂]
📸: Larisa K

Kuna viumbe wanaitwa Wakuja.
Wanaishi kwenye sayari yao ndogo iitwayo Kuja.
Wao pia wanautamaduni & maendeleo yao.
Mwaka jana, Wakuja waligundua uwepo wa sayari yetu ya Dunia.
Walipotuona binadamu👪, wakabaini kuwa tunaakili sana. Basi wakaanza kutufuatilia 🔭 ili kujua maisha na siri zetu.
Jumapili, Wakuja waliona hali isiyo ya kawaida duniani. Wakamtuma Mpelelezi wao kufuatilia kwa umakini kinachoendelea. 

Sasa ndio mpelelezi yule anapeleka ripoti kwa mfalme.Anasema,
"Huko nimeona suala la ajabu. Kuna kiduara kidogo ambacho wanaume wenye afya walikikimbilia kwa kasi huku wengine wakiwafuatilia kwa makini"

"Walivyo na akili walishindwa kukikamata?"
Anauliza mfalme.

“Huwezi amini kila walipo kisogelea hawakukikamata ila walikipiga mateke. Na hata walipokikamata, ghafla walikiachia tena” anajibu Mpelelezi kwa adabu.

Kiduara cha Binadamu
📸: Michal Jarmoluk

“Mhhh! Maajabu haya!” Mfalme anawaza.
Mpelelezi anaendelea kuwasilisha ripoti.
“Binadamu na viongozi wao walishangilia,kuogopa,kuomba Mungu na hata kulia wenzao walipokikimbiza na kukipiga mateke kiduara kile”
 
Mfalme anazidi kushangazwa na habari hizo za binadamu na kiduara. Anamuamuru mpepelezi kukisaka kwani kinaonekana kuwa na siri yao kubwa.
"Ukiweza kukileta kiduara hiko huku Kuja,nitakupandisha cheo na kukuweka mkono wangu wa kuume”
Anaahidi Mfalme kwa sauti ya Mamlaka!
 
Mambo yanazidi kuwa mengi!😂😂

Comments

Popular Posts

001.MWANZO

015: UGUMU WA URAHISI

017: KIPINDI CHA MASHAKA

016: SALA YA KUOMBA KIFO CHEMA.

014: KUHUSU MAKOMWE

013.CHASING WEMBLEY

012.KIPAJI SI UMAARUFU WALA PESA

005.KUNJUA MKONO