008.WATU WANABADILIKA
"People change, and forget to tell each other", aliwahi kusema Lilian Hellman.
Siku kadhaa nyuma, nilikwenda kuonana na rafiki yangu wa muda mrefu ambaye hatukuwa tumekutana kwa kitambo kirefu pia.
Ulikuwa wakati mzuri:tukiongelea yaliyopita, yaliyopo na yajayo.
Halafu nilimpelekea Karanga za mayai.
Kumbukumbu zangu zinajua kwa hakika kuwa huwa anazipenda!😋
So here comes the parcel and he says:
“Ohooo! Hapa sijui tunafanyaje sasa?!” sura yake ikionesha kufadhaika😞
“Vipi?” Nikauliza.
“Siku hizi sili karanga wala mayai.Nilidevelop allergy navyo.Nikila naugua kabisa. Niliumwa hapa kati, we acha tu. Yani ndo nimeshtuka kuwa sikuwahi kukwambia" Akasema.
Kulikuwa na ukimya mfupi kidogo. Kila mmoja akitafuta neno sahihi la kutamka baada ya taarifa ile. Tulijua kuwa nilipaswa kuambiwa lakini haikuwa hivyo. Nilinyimwa fursa ya kutimiza wajibu wangu wa kumpa pole na kumuombea apone haraka.
Nikafanikiwa kuwa wa kwanza kuuvunja kwa hatimaye kumpa pole iliyochelewa sana na kumsanifu kuwa anamkosi wa kupenda vitu visivyomfaa.
Tukacheka.Kauli ile ilitukumbusha jambo ambalo hapa sitoliongelea😂
Akatumia dakika kadhaa kunihadithia vizuri ilivyokuwa na anavyoendelea. Kuna namna ni kama alikuwa ananiahidi kuwa hatosahau tena kuniambia. Baada ya muda tuliendelea na story nyinginezo na akaniuliza;
“Umeuona wimbo mpya wa dada yako Yemi Alade?
[Kutokana na kumbukumbu zake,alikuwa anajua kwa hakika kuwa ninapenda nyimbo za msanii huyo. Yeye pia alizoea kumtaja kama Dada yangu kwani katika uhalisia, Yemi amezaliwa tarehe moja na dada yangu wa kuzaliwa😁]
Swali lile lilinikumbusha mbali.Tukiwa marafiki wadogo:wenye nafasi ya kuambiana na kukumbuka mwingine alichokipenda.
“Hee! Hivi yupo? Nina muda mrefu sijamfuatilia.”
Nikamjibu.
“Acha basi? Usiniambie na wewe umedevelop allergy nae?
Akasema kwa mzaha.
Watu Tunabadilika👥
Taratibu kuliko tunavyotaka ila haraka kuliko tunavyodhani.
Ubaya wa mabadiliko ni jinsi yanavyowatisha marafiki zetu na wengineo wanaotufahamu kwa karibu.
Yanawafanya washindwe kutukadiria au kubahatisha tunachowaza na kutamani
Kuna namna yanaturudisha tena kuwa kama watu tusiofahamiana😕.
Changamoto iliyopo ni kuwa ni vigumu kuwazuia watu kubadilika.
People meet a lot of new things to keep living the same life and dreams all years.
Kwa sababu zilizondani au nje ya uwezo wao,wanajikuta wameshabadilika.
Tupunguze kufikiri tunawajua sana kama mimi na karanga zangu za mayai.
Ndio, surprise ni nzuri ila ni vyema ukifanya updating ya unachoamini wanakitaka.
Saa nyingine waulize wanachoota kukamilisha, wanakotamani kwenda na wanachoamini kuhusu maisha bila kutarajia wakupe jibu lile lile kila mara.
PS:Tulikula zile karanga.He insisted it won't do any harm.
Tukasikiliza pia na wimbo mpya wa dada yangu Yemi Alade.
I think she still sings well but doesn’t sound the same. Inaonekana naye pia, AMEBADILIKA😂

Comments
Post a Comment