007.USHAURI SI KWA AJILI YA ANAEPEWA
Kwa kawaida mengi huwa yanaandikwa ushauri.Tena kwa herufi kubwa zilizokozwa.
Mfano: SMOKING KILLS.GET HELP TO STOP SMOKING.
Ukiangalia mapakiti yale,unaweza sema wanaozitumia wataelewa na kuacha.Lakini wote tunajua kuwa bado wanaowashauri wanatengeneza na wanaoshariwa wanazinunua.
Kwani kufa ndio nini? Mbona hata wasiovuta sigara wanakufa!
Wahusika wamekataa ushauri ule.
Tabia hii ya kukataa ushauri sio tu kwa wavuta sigara ila wengi wetu tunayo pia.
Tukipewa ushauri, iwe baada ya kuuomba au kwa kiherehere cha mtoaji😹,tunakuwa wagumu sana kuufuata.Hasa ushauri wa kuacha tunachokitaka au tunachokifanya tayari.
Aliyeambiwa ‘Hio biashara ngumu usifanye’, ndio anaelekea TRA kuisajili🏃
Aliyenong’onezwa ‘Huyo mchumba hakufai’, ameamua kuitisha kikao cha posa💍
Ukiangalia vizuri,utagundua kuwa watu hawashauriki kirahisi🚫
Ushauri unakuwa tu sehemu ya mchakato ila wanachotaka kukifanya tayari wanacho kichwani na moyoni.
Lakini miaka nenda rudi, kushauriana kumebaki kuwa sehemu muhimu ya maisha yetu kwa sababu kihalisia, ushauri ni kwa ajili ya anayeutoa na wanaousikiliza si anayepewa.
Wakiufuata na ukawasaidia,the better!👌
Wakiuacha,may they defy the odds!🤞
Lakini angalau ulipata nafasi ya kueleza ungekuwa katika nafasi yao ungefanyaje.
Ukitoa suala la kutimiza wajibu,sometimes kuna wale wa pembeni wanaousikia. Hawawi under pressure kwa hio wanauelewa na kujifunza zaidi.
Ushauri wa kuwa sigara inaua, unatuzuia wengi sana tusiingie kwenye uvutaji kuliko unavyowatoa ambao tayari wanavuta.
A lot of other advice work just the same way!
Ninachojaribu kusema ni kuwa tusiache kuwashauri marafiki,kaka,dada,wadogo zetu nk.Hata tunapojua wazi kuwa wanaweza kutotusikiliza👎
Ni sehemu muhimu ya mahusiano yetu:Kustahimili kushudia wakifanya kinyume kabisa na tulivyowashauri na bado tukawa na uwezo wa kuwakumbatia wakimaliza…
Tukisubiri watuambie👂;
“Si unaona,sijakusikiliza ila nimefanikiwa” 😁
Au
“Nisamehe.Ningejua ningekusikiliza”😞

😁
ReplyDelete