006.NJIA ZA KUTUMIA WATU

 Mwenye kovu,Usidhani Kapona.
"Naomba mnisaidie kubeba mizigo yangu"

Ukitaka kuwatumia watu kwenye shughuli zako,kuna njia nne za haraka haraka unazoweza kupita.

1. UWALIPE [Hela/Maarifa/Wakutumie pia]
2. UISHI NAO VIZURI [Kirafiki/Kindugu nk]
3. UWE MFANO KWAO [Watamani kuwa kama wewe]
4. _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _ _
 
Lakini tupo baadhi tunaotaka “kuwatumia” wengine bila kufanya lolote kati ya hayo matatu. Hata hilo la 2 lililorahishwa sana na Bwana Simu, tunashindwa.

Unanamba yake ila kusalimiana ni hadi yeye aanze na hapo ulijibu text yake ya Merry Christmas kipindi cha Pasaka๐Ÿ˜†
Anabirthday,hujamuwish๐Ÿค
Amefiwa, hamna pole๐Ÿค
Amevaa joho,umeuchuna๐Ÿค
Amepost kichekesho, hata emoji za kucheka hujatuma ila kimekuchekesha mpaka tumbo limekuuma๐Ÿค

Ghafla unaibuka kutoka mafichoni na salamu ya mchongo halafu unamdondoshea ombi la mchango, mkopo au link ya shughuli zako, akusaidie kushare.
Makwazo hayana budi kuja lakini ole wake mtu yule ayasababishaye! 

Wapo watu hawana roho za kwa nini na wanakuchangia au kushare vitu vyako kama ulivyoomba halafu unarejea kwenye mchezo ule ule.
Kesho ukirudi tena unadhani watakubali?

Njia namba 4.

Unataka kuwatumia watu na zile njia 3 huzitaki?
Kuwa makini sana maana bila kujijua unaelekea kufuata ile njia iliyobaki.
4.Kutumia nguvu za giza.Uwageuze vikaragosi, wapige kazi!

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

 
 
 

Comments

Post a Comment

Popular Posts

001.MWANZO

015: UGUMU WA URAHISI

017: KIPINDI CHA MASHAKA

016: SALA YA KUOMBA KIFO CHEMA.

014: KUHUSU MAKOMWE

013.CHASING WEMBLEY

012.KIPAJI SI UMAARUFU WALA PESA

005.KUNJUA MKONO