004.MPOTEANO
Waliohai,hawaachi kuonana.
![]() |
| "Ndugu yangu umepotea!" 📸: Meir L |
Wiki iliyopita Aunty yangu alinipigia simu📲 jioni kunijulia hali.
Nilipoona jina lake wakati simu inaita,nilishtuka na kufurahi😃
Unajua mchana nilimkumbuka sana na nikasema nikitulia nitampigia. Hekaheka ziliponizidi, nikasahau.
Nadhani hata wewe umewahi kumkumbuka mtu halafu na yeye akakukumbuka.
Sasa kuna kitu nimeamua kukiita Mpoteano.
Mpoteano ni muda unaoweza kukaa kabla ya kumtafuta mtu kumsalimia au kumuona baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho.
Inaweza kuwa siku,wiki,miezi au hata mwaka.
Mpoteano ukishatimia,akili inakukumbusha kumhusu.
Inaweza kutafuta sababu kama vile kukuonesha mtu wanayefanana au akakujia tu akilini, paap!💥
Huna shida naye zaidi ya “Habari za huko?”
Ukimkumbuka kwa sababu unachangamoto fulani na unadhani atafaa kukusaidia, huo si Mpoteano🚫😂
Mipoteano inaweza kulingana au kutofautiana.
Yawezekana mpoteano wangu na wa Aunty unafanana. Nilipoanza kukinai kukaa bila kumjulia hali na yeye akawa ametosheka😊
Muda mwingine unaweza kuwa na mpoteano mdogo kwa mtu ambaye anampoteano mkubwa kwako.
Basi unajikuta unakuwa wa kwanza kumtafuta mara nyingi au zote.
Sounds familiar? 😂
Lakini mara nyingi mipoteano inatanuliwa kwa viburi😤 na madeni💰
~Ndio unanijia akilini mara kwa mara ila sikutafuti tu.Wewe pia mbona hunitafuti? Huna simu?
~Au unanidai:Sasa tusalimiane nini wakati mpango wa kukulipa sina?
Umeona mambo hayo!? 😂
Anyways,mipoteano ikiwa mirefu sana,ndio mwanzo wa kupoteana mazima.Kwa hio tujitahidi kuifupisha ili baaada ya haya yote,Tupatane!

Comments
Post a Comment