003.MARA ZA MWISHO

Hakuna refu lisilokuwa na ncha


"Hatujamalizaaa!"

Kuna siku ilikuwa mara ya mwisho Mama kutubeba mgongoni au Baba kutuweka mabegani:bila wao wala sisi kujua.
Walipotushusha hawajawahi kutupandisha tena 🔚
Labda siku ile wangejua kuwa ndio tamati:wangetubeba kwa muda mrefu zaidi nasi tungejishikilia kwa hisia kali😍
Nadhani tungepiga na picha ya ukumbusho📸

Kuna siku ilikuwa mara ya mwisho kuvaa ile nguo au kwenda ile sehemu.
Ilikuwa mara ya mwisho kusimama mstarini,kukaguliwa usafi wa meno na kucha.
Kuna siku ilikuwa mara ya mwisho kumuona  mtu yule kwa hisia ile.
Sasa ukimuona,humuoni tena vile.
Kuna kitu hukihisi kabisa💔 au unakihisi zaidi 💘

Inaonekana maisha yana mara za mwisho nyingi, zinaozoishia kila siku bila sisi kujua.
Hata jana nikiwa na marafiki, mmoja akasema:
“Kuna siku itakuwa mara ya mwisho kuchana hizo nywele. Baada ya kunyoa, unashangaa tu hazioti tena”
Tulikuwa tunaongelea kuja kwa uwalaza👴😂
 
Tukacheka;na moyoni nikakumbuka usemi wa kuwa mwisho wa jambo moja ndio mwanzo wa jambo jingine.

Comments

Popular Posts

001.MWANZO

015: UGUMU WA URAHISI

017: KIPINDI CHA MASHAKA

016: SALA YA KUOMBA KIFO CHEMA.

014: KUHUSU MAKOMWE

013.CHASING WEMBLEY

012.KIPAJI SI UMAARUFU WALA PESA

005.KUNJUA MKONO