002.TULIKUNUNUA UKIWA KWENYE KIKAPU
Ni jibu ambalo watoto wengi hulipata wanapowauliza wazazi wao walipowatoa.
Mimi pia nilikuwa mmoja wao. Na nilikaa muda mrefu nikisadiki kuwa watoto wananunuliwa wakiwa kwenye vikapu😂
Oh my God!😃 Exactly what they were looking for.
A Calm Black Boy!
Hadithi hii ilikuwa inanipa raha fulani hivi😊
Kwamba katika kundi la watoto wengi nilichaguliwa.
Wazazi wangu walinichukua kwa ridhaa yao hata baada ya kutuona wengi wetu.Kuna kitu special walikiona, au sio?😃
Vyovyote vile but it was a perfect ego buster!
Umri fulani unapofika, watoto wanagundua walipotoka na wanapunguza kusema wanapokwenda.
Hatimaye siri kuhusu kuzaliwa ilivuja na nikainasa👊.
Kusema ukweli, sikuvutiwa nayo😣
Kumbe hakuna kuchaguana?😳 Na utakayempata, Umpende, Usimpende, UTAJIJU!? 😲
Kwa hio usikute kungekuwa na uchaguzi wa kwenye vikapu kama walivyonihadithia, labda wasingenichagua.
Usikute wangechagua mtoto mweupe na mchangamfu,
I foolishly thought!🙈
Kumbe ni jasho😰,machozi😭 na damu🩸. Na hata tumefika hapa tulipo kwa sababu kimsingi walitutaka💕
Ingekuwa hawakututaka, wangeweza kutugeuza takataka🚮
"Tuwaheshimu Baba & Mama👪, tupate miaka mingi na kheri duniani" inasema amri ile pekee yenye ahadi.
Wamejitoa sana na bado hawataki majivuno, wanarahisisha kwa kusema “Tulikunua ukiwa kwenye kikapu”
Who ever said parents are our 2nd God, I second him🤝

Comments
Post a Comment