017: KIPINDI CHA MASHAKA
why such a long face? I am sorry to break the news but unfortunately, I don't have the desirable content for my audience. The blog is struggling to remain relevant to the majority of its readers. Watu wengi wanaosoma blog hii ,kwa sasa wanataka kusikia juu ya mambo ambayo sina uzoefu,busara wala mamlaka ya kuyazungumzia. Unajua, hadhira yangu kubwa ni watu na hasa marafiki zangu nilionao rika moja.... Sehemu kubwa ya rika hili, ndio inaanza rasmi kuingia kwenye kipindi cha mashaka maishani mwao. Kipindi hiki kimetawaliwa na tamaa za kutisha,mabadiliko ya kushangaza na maswali mengi yasiyo na majibu ya Ndio/Hapana. Si rahisi kuyajibu! Nitapataje kazi?--Napataje pesa? Niki zipata niwekeze kwenye nini? Nik a ishi mkoa/nchi gani? Nitajuaje mchumba niliyenae ananifaa?-Au nampataje ikiwa sina? Baada ya miaka kadhaa ya balehe kali iliyotuaminisha tunajua kila kitu na tusiambiwe chochote na yeyote; Kipindi cha mashaka kinapoingia,tuna...